Uhakiki wa Shutdown Academy Ya Advocacy Assembly katika mwaka wa 2023

Katika mwaka wa 2023 Shutdown Academy ya Advocacy Assembly ilifanikiwa sana katika kuendeleza upiganaji wa haki za kidijitali na kupigania haki za uzimaji mtandao kote ulimwenguni. Tuna furaha kushea na nyinyi mafanikio makubwa na miradi tulifanikisha mwaka huo, na kuonyesha shughuli ambazo tumefanya kwa muda wa mwaka mmoja.

Kurahisha Ufikiaji: Uzinduzi wa Tofuti ya Lugha-nyingi 

Kuanzia mwaka huu, tulijitahidi kupunguza vizuizi vya lugha na tukaongeza lugha tatu mpya - Kireno, Swahili, na Kifaransa - katika tovuti yetu. Kwa kuongeza lugha zetu, tunatoa kozi zetu sasa katika lugha saba, kutuwezesha kufikia watu wengi.

 

Mafanikio Makubwa: Kozi 10, Lugha 7

Mojawapo ya mafanikio ya mwaka 2023 ni kuzinduliwa kwa kozi kumi zote katika Shutdown Academy, ambazo ziko katika lugha saba sasa. Mafanikio haya ni muhimu katika juhudi zetu za kuwezesha upatikanaji wa kontenti zetu kwa kila mtu na kuwezesha wanaharakati kote duniani.

 

Kuwezesha Watetezi: Mradi wa Mafunzo ya Ukuzanaji

Kuanzishwa kwa Mradi wa Mafunzo ya Ukuzanaji ulipokea mapokezi mazuri, kwa maombi 1,060 kutoka nchi 135. Huu ulikuwa mradi wa kujumuika wa wiki-7 kuwapa ujuzi viongozi na wanaharakati ili kugana dhidi ya uzimaji. Kutokana na mafanikio ya mradi huo tumeamua kutangaza kuurudisha kuanzia Februari hadi Aprili 2024. Tafadhali angalia hii linki kwa taarifa zaidi. 
 

Kutambulika Ulimwenguni: RightsCon 2023

Advocacy Assembly's Shutdown Academy ilishiriki RightsCon 2023 na iliwehusishwa katika mikutano mingine kama OONI, IODA na Access Now.
 

Mijadala Miwili ya Wataalam kuhusu Utaratibu wa Kisheria  na Simu za Setilaiti

Kama mojawapo wa Mradi wa Mafunzo ya Ukuzaji, tuliandaa mijadala miwili ya wataalam. Mmojawapo ulihusu utaratibu wa kisheria dhidi ya uzimaji mtandao, ambao uliangazia changamoto na nafasi zinazohusika katika utaratibu wa kisheria. Mjadala mwingine ulifahamika kama “Mjadala kuhusiana na Jinsi ya kutumia Simu za Setilaiti” na tukaangazia haja ya kuwa njia nyingine salama za mawasiliano wakati mtandao umezimwa kutokana na mizozo na uangalizi wa serikali. Tulisisitiza umuhimu wa kutumia simu za setilaiti vizuri ili kuimarisha uhusiano ulimwenguni, hasa wakati mtandao umezimwa kwa muda mrefu.

 

Kozi za Uanahabari wa Data kwa raia wa Iran

Mwaka 2023, tulishirikiana na Iran Open Data kuzindua kozi mbili za Unahabari wa Data kwa Kifarsi

 

Advocacy Assembly katika FIFAfrica: Warsha jinsi ya Kupigana na Uzimaji wa Mtandao

Kushiriki kwetu katika Kongamano la Uhuru wa Mtandao Barani Afrika ((FIFAfrica 2023), ilijumuisha kuandaa warsha kuhusu Shutdown Academy na mbinu za kupigana na uzimaji wa mtandao. Ushirikiano huu ulituwezesha tukaungana na watetezi jijini Dar-E-Salaam, kusaidia kwenye juhudi za pamoja dhidi ya uvurugaji wa mtandao.

 

Zanakazi

Advocacy Assembly ilichapisha zanakazi mbili mwaka 2023—zanakazi ya kwanza iliangazia mwongozo wa kisheria kuhusiana na vikwazo vya kimtandao na uzimaji barani Africa. Ya pili, ambayo iliundwa na Access Now "Kurudi kwa Dhuluma za Kidijitali", inapatikana sasa katika lugha zote saba, ikijumuisha including Swahili, Kireno, na Kifaransa.

 

Kutazamia mwaka wa 2024

Tunapoangazia mafanikio ya 2023, Advocacy Assembly inalenga mafanikio zaidi mwaka huu. Tarajia mradi wa pili wa Mradi wa Mafunzo ya Ukuzaji na pia zanakazi yetu mpya, ambayo itaangazia madhara ya kiuchumi kunapozimwa mtandao. Kwa pamoja, tutaendelea kuunga mkono haki za kidijitali na kuweka juhudi za uwazi pamoja na ulimwengu uliojumuika pamoja.

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

Blogu

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo